BENKI Kikuu Tanzania (BoT), imesema imeamua
kuchukua usimamizi wa benki ya Twiga (Twiga Bancorp Limited), kuanzia Oktoba 28
mwaka huu.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa
benki ya Twiga ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwaya sheria ya
mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo, Gavana wa BoT, Prof. Beno Ndulu, alisema upungufu huo wa mtaji
unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za benki kwa benki ya Twiga kuhatarisha
usalama wa amana za Wateja wake.
Alisema kutokana na uamuzi huo, BoT,
imesimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa benki ya Twiga na imemteua
Meneja Msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za Benki Kuu.
Prof. Ndulu, alisema pia umma unaarifiwa kuwa
katika kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki moja, kuanzia leo, shughuli za
utoaji wa Huduma za kibenki za benki hiyo ya Twiga zitasimama ili kutoa nafasi
kwa ajili ya kupanga taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.
Alsema BoT, inauhakikishia umma kuwa itaendelea
kulinda masilahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu
katika sekta ya fedha.
0 comments:
Post a Comment