Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki
cha Stella Marios cha Mtwara Padre, Dkt. Charles Kitima akichangia mada katika
moja ya Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere.( PICHA
KUTOKA MAKTABA)
Na: Frank Shija, MAELEZO
Uanzishwaji wa Bodi ya Ithibati
ya Wanahabari kama ilivyoainishwa katika Muswada wa Huduma za Habari wa mwaka
2016 hautaminya uhuru wa kutafuta na kusambaza habari.
Hayo yamebainishwa na Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Marios kilichopo Mtwara Dkt. Charles Kitima
katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo.
Dkt. Kitima amesema kuwa msingi
wa haki ya kutafuta taarifa na kusambaza habari unatokana ibara ya 18 ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo watu wasiwe na hofu ya kuwa Bodi hiyo
itawaminya watu kutoa mawazo yao.
“Bodi ya Ithibati ya Wanahabari
haiwezi kuwa kizuizi cha watu kutafuta na kusambaza habari kwani haki hiyo ipo
kikatiba kupitia ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Alisema Dkt. Kitima
Amesema kuwa haoni sababu
yoyote ya kupinga uanzishwaji wake kwa kuwa malengo yake ni kuhakikisha
inasimamia kanuni za maadili ya wanahabari hapa nchini na kuijengea heshima
tasnia.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na
kuanzishwa kwa Bodi hiyo hakuna maana kwamba uanzishwaji wake utachukua
majukumu ya taasisi zingine za habari zilizopo na kuongeza kuwa waandishi wa
habari duniani kote wanafanya kazi kwa kufuata miiko ya maadili ya uandishi wa
habari.
Alisema kuwa suala kubwa kwa
mwanahabari ni kuzingatia maadili na weledi wa taaluma yake ili kutekeleza
majukumu yake pasipo kusababisha usumbufu kwa mtu au kikundi kingine.
Bodi ya Ithibati ya Wanahabari
ipo katika muswada wa huduma za Habari sehemu ya Tatu na kuelezewa kwa kirefu
katika kifungu cha 10 hadi 20 katika muswada huo unaopatikana katika Tovuti ya
Bunge ambayo ni www.bunge.go.tz.
0 comments:
Post a Comment