Na Ally Daud-Maelezo

Hayo yamesemwa naKatibuMkuuwaWizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano Prof. FaustinKamuzora wakati wa kukabidhi matokeo ya utekelezaji wa mradi kwa vijana wa mafunzo ya mambo ya Tehama na habari ambao umejumuisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao umefanyika jijini Dar es salaam.

“Vijana wanatakiwa wawe wabunifu ili waweze kutumia fursa zilizopo kwenye Nyanja za uchumi wa Tehama kwa ujumla ili waweze kunufaika na ubunifu wao kwa kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla” alisema Prof. Kamuzora.

Aidha Prof. Kamuzora amesema kuwa mradi huo ambao umefanyika kwa makubaliano  ya Finland na Tanzania umegharimu kiasi cha fedha za Euro milioni 6 utakamilika rasmi ifikapo Desemba mwaka huu ili kuweza kutoa fursa kwa vijana kuchangia uchumi wa nchi katika sekta ya mawasiliano.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano wa Wizara hiyo Bi. Clarence Ichwekeleza alisema mradi huo umelenga kuwapa vijana mafunzo  ya jamii habari ili kusaidia taifa kufikia katika uchumi maarifa ambao utatokana na maendeleo ya Tehama.

“Watanzania hususani vijana wanatakiwa kupata ujuzi wa Tehama na kuwa na uwezo wa Jamii Habari ili kuweza kuendelea kiuchumi kwa kupitia maendeleo ya mawasiliano ili kuweza kuwa na uchumi maarifa ambao ndio unaofanyika duniani kote hasa kwa nchi zilizoendelea” alisema Bi. Ichwekeleza.


Mradi huo ambao umewalenga vijana kutoka katika sekta  ya Tehama umefanyika  kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Finland umeanza mwaka 2011 na kutarajiwa kufikia tamati kwa kukamilisha malengo yake Desemba mwaka huu.

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top