![](https://scontent-mrs1-1.xx.fbcdn.net/v/t1.0-0/p480x480/14601095_1316006645108532_8224604355912568181_n.jpg?oh=34b7eae892af127707faaaba94bc11fe&oe=5899E836)
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Timu ya
Yanga imeshuka bila ya Kocha Pluijm,aliyeachia ngazi kwenye uwanja wa
Uhuru jijini Dar es salaam wakiwa chini ya Mwambusi vijana wa jangwani
wameng’ara zaidi kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu
na kufanya timu hiyo kuwa na mabao 10 kwa michezo miwili ikumbukwe
walimfumua Kagera 6-2.
Yanga
waliandika goli la mapema dakika ya 6 likifungwa na mshambuliaji Obrey
Chirwa baada ya makosa ya walinzi wa Ruvu kujichanganya na kumkuta
mfungaji akiwa katika nafasi nzuri ya kuiandikia goli huku likiwa goli
la tano kwa Chirwa ambaye ameendelea kung’ara kila mechi.
Baada ya
kufungwa goli hilo timu zote ziliendelea kupata nafasi nyingi za wazi na
kushindwa kupata magoli mengi zaidi huku kiungo cha kati cha wanajeshi
hao kikipotea kabisa hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele.
Kipindi
cha pili kilianza kwa wenyeji Yanga kukosa nafasi za wazi kupitia kwa
Donaldo Ngoma pamoja na Msuva baada ya kuona hivyo Kocha Mwambusi
alimtoa Ngoma dakika ya 54 na nafasi yake kuchukuliwa na Amis Tambwe.
Dakika ya
63 Tambwe aliiandikia Yanga goli la pili na likiwa la tano kwake baada
ya kuichambua ngome ya Ruvu na kuwafanya wapotezee zaidi na kukubali
kuendelea kushambuliwa kama nyuki Simon Msuva alifunga la tatu mnamo
dakika ya 82 naye likiwa la tano msimu huu wa Ligi.
0 comments:
Post a Comment