Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mhe William Lukuvi akikabidhi cheti kwa mwakilishi wa makampuni kama ishara ya kutambua mchango wao katika kuwezesha mkutano  mkuu huo wa kwanza na kongamano la wapimaji, kushoto kwake ni mkurugezi wa upimaji wa Ramani bw Justo Lyamuya  mapema hii leo jijini Dar es salaam.

Na Frank wandiba.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi, amesema, asilimia 85 ya Ardhi nchini haijapimwa, hivyo kufanya wakazi katika miji kuendelea kuishi kwenye makazi holela.

Mhe Lukuvi, aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, kuwataka wataalam hao, kufanyakazi ya upimaji ardhi kwa uadilifu ili kuondokana na makazi holela nchini.

Alisema, kutokana na sehemu kubwa ya ardhi kutopimwa, hali hiyo imekuwa chanzo kikubwa kwa serikali kupoteza mapato ambayo kama yangekusanywa yangesaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye jamii
Lukuvi, alisema kutokana na mazingira hayo serikali imewaagiza wataalamu hao kujipanga na kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wawe wamepima ardhi yeny ukubwa wa viwanja zaidi ya 400.

Aidha, Lukuvi alisema nia ya serikali nikuona inafanikiwa katika miaka 10 ijayo kwa kila mtu ana kuwa na hati ya kiwanja au shamba lililopimwa
Aliongeza kuwa wakati umefika wa kuondokana mfumo wa kizamani wa uandaaji wa hati za karatasi na baadala yake lazima wataalamu watumie mfumo wa kieletroniki katika umimaji wa ardhi ya wananchi.

Alisema mfumo huo wa kisasa utasaidia kuzuia wananchi kudhulumiwa ardhi na baadhi ya watu wenye uroho wa ardhi kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu
Washirki wa kongamano hilo wakimsikiliza mgeni rasmi mhe William lukuvi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano mkuu na kongmano la wapimaji ardhi ampema leo jijini Dar es salaam
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mhe William Lukuvi akitembelea mabanda ya washiriki wa mkutano huo kujionea vifaa mbalimbali vya kisasa vya upimaji wa ardhi

"Ni marufuku kwa wapimaji ardhi walioajiriwa na serikali kuwa na kampuni za upimaji wa ardhi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuondokana na mgongano wa kimasilahi kati yao na kampuni binafsi,"alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema wapimaji wa sekta binafsi wamekuwa wakifanya vizuri ukilinganisha na wale ambao wameajiliwa na serikali.

Naye Rais IST, Martins Chodata alisema kuwa wamejipanga vizuri na kuahidi kuwa watashirikiana serikali katika kazi hiyo ya upimaji ardhi.

Alisema, kuwa hawatakubali kushirikiana na baadhi ya wapimaji ardhi ambao wamekosa maadili na wanaosababisha migogoro nchini.




Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top